Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kaimu waziri wa mambo ya nje wa Sudan Omer Gamar-Eddin amesema kupitia taarifa kuwa wizara yake haikujadili uhusiano na Israel. Aidha amesema msemaji wa wizara hiyo Haidar Badawi al-Sadiq hajapewa idhini ya kutoa kauli yoyote kuhusu suala hilo.
Kauli hiyo imekuja huku Umoja wa Falme za Kiarabu ukiendelea kukosolewa vikali kutokana na hatua yake ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Kufuatia hatua kadhaa zilizochukuliwa na Rais Donald Trump wa Marekani kwa lengo la kurahisisha uanzishwaji wa uhusiano wa kawaida kati ya Imarati na utawala haramu wa Kizayuni, Alkhamisi iliyopita pande mbili za Abu Dhabi na Tel Aviv zilisaini mkataba na kuafikiana rasmi kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia.
Makubaliano hayo kati ya Israel na Imarati yamekabiliwa na wimbi kali la malalamiko na upinzani wa makundi ya Palestina, nchi za eneo la Asia Magharibi na shakhsia kadhaa wa kisiasa duniani, ambao karibu wote wamesisitiza kwa kauli moja kuwa, hatua hiyo ya Imarati ni uhaini na usaliti kwa malengo matukufu ya Palestina.
342/